NICK MINAJ :PROFILE
Jina Kamili : Nika Tanya Maraj
Jina analotumia kimuziki : Nick Minaj
Mahali alipozaliwa :
Alizaliwa Saint James Trinidad na alipokuwa na umri wa miaka 5 alihamia New York City
Yeye ni nani :
Ni rapa, muimbaji, mtunzi wa nyimbo na muigizaji wa televisheni kutoka nchini Marekani
Kazi ya muziki alianza lini ? :
Kipaji chake kilionekana kati ya mwaka 2007 na 2009 wakati alipotoa nyimbo zake zilizowavutia Young Money Entertainment ambao waliingia naye mkataba
Aliyemvutia kuingia kwenye sanaa hiyo ya uimbaji:
Minaj alikiri kabla ya kuimba alivutiwa na Lisa Lopes "Left Eye", Lil Wayne, Lauryn Hill, Jadakiss, Natasha Bedingfield, Fox Brown, Lil Kim na Missy Elliott
Anao wakubali zaidi kwenye gemu :
Minaj alidai kuwakubali Jay Z, Foxy Brown na alishawahi kusema "nampenda sana Foxy kama rapa bora wa kike pia siwezi kukosa kumtaja Jay Z kama msanii bora wa kiume, tulipokuwa shuleni na wenzangu tulikuwa tukijifunza kuimba mistari ya Jay Z"
Kitu gani ambacho hawezi kusahau katika maisha yake? :
Minaj alidai kuwa hawezi kusahau kifo cha binamu yake Nicholas Telemaque ambaye alipigwa risasi karibu na nyumbani kwake huko Brookly, New York
Ananafasi gani ya utajiri :
Kwa mujibu wa Forbes ambayo hutoa tathimini juu ya uwezo wa wasanii ulimtangaza Minaj yupo katika matajiri kumi wa Hip Hop
Mwaka 2011 kwa mujibu wa Forbes Minaj alishika namba 8 kwa kuwa na utajiri unaofikia dola 15 milioni, kwa sasa utajili wake unaweza kuongezeka kutokana na mikataba kadhaa aliyoingia hivi karibuni
Maisha ya ugomvi :
Minaj alishawahi kuingia katika ugomvi na rapa Lil Kim baada ya rapa huyo kumtuhumu mwenzake kumuibia mistari yake kutoka katika kibao cha Pink Friday
Mbali na hayo hivi karibuni pia Minaj aliibuka katika ugomvi mwingine na muimbaji mkongwe Mariah Care
Gari la kwanza kumiliki :
Gari la kwanza kumiliki Minaj lilitokana na kuzawadiwa akiwa na umri wa miaka 19 baada ya kuchaguliwa kuwa muhudumu bora katika hoteli aliyokuwa akifanyia kazi
Kitu gani alikifanya cha ajabu? :
Alicheza picha ya ngono na kukiri hadharani huku akiwashauri wasichana kwa kuwaambia kuwa katika maisha ngono haiwezi kuepukika hasa kwa mabinti
Minaj ni wa aina gani ?
Ni binti mwenye msimamo na kuna wakati alishatoa nyimbo mbili ambazo zinawatukana wanaume moja kwa moja
Anaabudu dini gani?
Minaj ni muumini mzuri wa dini ya kikistro, alishawahi kusema kuwa roho yake ipo kwa yesu ambapo mara nyingi hutumia mistari katika biblia