PREZZO AWASHANGAZA MASHABIKI WAKE
BAADA ya mume wa marehemu Goldie kuibuka na kuziweka hadharani picha zinazoonyesha siku ya harusi yao na kudai kuwa uhusiano uliokuwepo baina ya marehemu mke wake na msanii wa Kenya Prezzo ulikuwa ni wa kuigiza tu na wa kuonekana kwenye 'Tv'
Kutokana na kitendo hiko baadhi ya wakenya waliamua kumtumia ujumbe Prezzo kupitia mtandao wa kijamii Twitter kuhusu hali ya kutoelewa siri iliyokuwepo kuhusu uhusiano huo, "Kumbuka wiki chache zilizopita kulikuwa na habari kila mahali kuhusu kutaka kufunga ndoa kati ya Prezzo na Goldie na sasa mwezi umepita sasa ukweli imegundulika kuwa Goldie alikuwa amefunga ndoa na mtu mwingine .
Mashabiki wameshindwa kuelewa kuhusu jambo hilo" aliandika Robert Alai.