PRO 24 DJ'S KUFANYA MAKAMUZI TBC ONE USIKU WA VALENTINE
Wakati baadhi ya watu wanafanya tasmini na kufikiria jinsi gani watakavyosherehekea na kuifanya siku ya wapendanao 'Valentine day'iwe ya kipekee na yenye utofauti, Pro 24 Djs kama kawaida wamejipanga kwa ajili ya kufanya shoo ya kipekee 'Crazzy Show' kwenye kipindi cha Bang na Pro 24 siku hiyo ya Alhamisi ambapo ni siku ya wapendanao
Kipindi ambacho kinarushwa kila siku ya alhamisi katika Televisheni Taifa ya (TBC one) kuanzia saa nne mpaka sasa saba usiku ambapo Crazzy Djs wanafanya video mix zenye radha tofauti tofauti ili kuukamilisha usiku wako
Dj Dea ni mmoja wa madj wa pro 24 ambao atafungua kipindi hiko kwa muda wa kwanza huku akipiga nyimbo zenye miondoko na radha tofauti tofauti
Pro 24 wameandaa usiku huo ili kuendelea kutoa burudani kwa mashabiki wake huku wakiwa wanapiga nyimbo yaani video mix tofauti tofauti zinazotamba duniani kote









