VALENTINE DAY
SIKU ya wapendanao (Valentine’s day) unaichukuliaje na umepanga kufanya nini ili kukamilisha siku hiyo ambayo ni kesho , Siku ya wapendanao limetokana na neno la kigeni (Valentine) lenye maana ya upendo, kupendana, kwa wapendanao.
HISTORIA SIKU YA WAPENDANAO
History ya siku hiyo imetokea Roma, Inaelezwa kwamba, siku hiyo huadhimishwa kama kumbukumbu ya Padre Valentino ambaye aliuawa na Utawala wa Kirumi uliokuwa chini ya Mfalme Claudia kwa kosa la kutetea waumini wake wafunge ndoa.
Ilivyo ni kwamba, Mtakatifu Valentino alikerwa na Utawala wa Kirumi ambao uliwakataza vijana kufunga ndoa na badala yake kwenda vitani, Kwa msingi huo vijana wakawa na vimada nje hivyo kwenda kinyume na utaribu na maagizo ya imani aliyoisimamia Mtakatifu Valentino.
Kwa sababu hakupenda hilo liendelee, akaamua kuendesha zoezi la kuwafungisha ndoa vijana kwenye mahandaki chini ya kanisa kwa siri kubwa hata hivyo, aligunduliwa na kufungwa na baadaye kuhukumiwa kifo.
Kwa msingu huo, kwa sababu Mtakatifu Valentino aliauwa siku na tarehe kama hiyo, ikatangazwa rasmi kuandhishwa kwa ajili ya kumkumbuka kama Baba wa Upendo – mtetezi wa wanandoa
Awali ilianza kuadhimishwa huko Roma, lakini baadaye ikaenea katika nchi za Magharibi na dunia nzima kwa ujumla. Wakati mapokeo ya kuadhimisha siku hii yalipoanza, ilionekana kama ni ya kidini zaidi, lakini baadaye ilipochunguzwa mantiki ya uadhimishaji wenyewe, ikaonekana kuwa na maana kwa watu wa madhehebu yote.
Aliyetangaza rasmi kuadhimisha siku hiyo ni Papa Gelasius, ambapo alisema ikumbukwe kama ishara ya kumuenzi mtetezi wa ndoa Mtakatifu Valentino.
UHIANO WA SIKU YA WAPENDANAO NA MITINDO
Mitindo ni sehemu ya maisha kila siku na siku ya wapendanao ni moja ya sehemu ya maisha hivyo lazima utengeneze kitu cha tofauti kinachondana na siku hiyo
Katika upande wa mitindo rangi nyekundi inatumika kila siku ingawa kwa siku ya wapendanao inakuwa maalum kwa ajili ya kutimiza siku hiyo, inaweza ukatumia mitindo tofauti tofauti ili kuendana na rangi hiyo
Siku ya wapendanao unaweza ukatumia vitu mbalimbali vyenye rangi nyekundu kuonyesha ishara ya upendo kuwepo mahari hapo wanaopenda kuishi maisha ya mitindo lazima siku hiyo waifanye iwe tofauti kuanzia muonekano wa mavazi na si mavazi peke yake hata jinsi ya kupanga vitu mahali unapoishi
Kwa siku hiyo rangi nyekundu zitaenea sana katika mavazi, kwa upande wa maofisini pia unaweza ukavaa nguo nyekundu ikumbukwe kuwa si lazima uvae nguo yenye rangi hiyo ila unaweza pia ukachanganya rangi ingawa nyekundu itaonekana
Unaweza ukabana kibanio chekundu, chini ukavaa siketi ya rangi ya kijani ambayo pia ni rangi ya mwaka na shati la mtindo wa 'high low' lenye rangi nyekundu ukaonekana umependeza na kuvutia zaidi
Ifahamike kuwa unaweza ukavaa kitu kimoja chekundu na si lazima kuonekana kuvaa nyekundu kila kitu kwani unaweza chagua kuvaa hata hereni za rangi hiyo na bado ukaonekana kuvutia zaidi, hali kadharika kwa upande wa kutoka usiku na yule umpendae hapo sasa ndipo usipokuwa makini unaweza ukajikuta unachemsha
Kuwa makini na aina ya nguo unayochagua kuvaa kwani unaweza ukavaa gauni 'high low jekundu kiatu kirefu kinaweza kikawa chekundu au cheusi
Katika kuchanganya rangi inabidi kuwa makini ila rangi nyekundu inaendana na rangi ya kijani, blue pamoja na nyeusi inakufanya uonekane mrembo na unavutia zaidi
KUNA MAHUSIANO GANI YA SIKU HIYO NA TENDO LA NDOA
Baadhi ya watu wamepoteza maana halisi ya siku hii muhimu kwa wapendanao na kuibadilisha kuonekana ni siku ya kufanya ngona na isitoshe wengine wanafanya ngono zembe
Baadhi ya watu wanahisi kuwa ni siku ya kufanya mambo yasiyofaa Kwao, wapendanao ni ngono tu na isitoshe wengine wanaanzisha uhusiano siku hiyo kwa lengo la kupata mtu wa kustarehe naye hili ni kosa.
Pia kuna baadhi wamekuwa wakifanya vurugu na kila aina ya uchafu Si maana halisi ya siku hiyo, hii ni siku ya kuonyesha namna mnavyopendana na kuthaminiana, kitu cha msingi hasa hapa ni pendo la kweli.