Google PlusRSS FeedEmail

SWAHILI FASHION WAANDAA ONESHO



SWAHILI fashion wiki (SFW) katika kuendeleza tasnia ya sanaa ya ubunifu na kuongeza kasi ya maendeleo ya tasnia ya mitindo nchini Tanzania imeandaa onyesho la mavazi Afrika Mashariki na kati litakalofanyika visiwani Zanzibar ambapo wabunifu nguli kutoka Tanzania bara na Zanzibar wataonyesha ubunifu wao

Katika tukio hilo wabunifu zaidi ya kumi wataonyesha mavazi huku wakitangaza dhana nzima ya kujali vitu vinavyotengenezwa Afrika hususani Tanzania ili kutangaza Tanzania na rasilimali zake (Promote Made in Africa Concept)

Hayo yalielezwa na muanzilishi muandaaji wa SFW Mustafa Hassanali jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati ya onyesho hilo kuwa ni kutangaza na kuinua vipaji vya wabunifu wa hapa nyumbani

Alisema kuwa Kupeleka SFW  kwa mashabiki waliopo visiwani Zanzibar, ni kuendeleza utamaduni wa nchi yetu pamoja na kuwa na tukio bora la burudani na biashara katika tasnia ya mitindo

Alisema kuwa onyesho hilo litawashirikisha wabunifu nguli toka bara na visiwani kuonyesha ubunifu na ladha tofauti za kiutamaduni hali ambayo itasababisha mashabiki wa ubunifu na mitindo kupata ladha kutoka kwa wabunifu wa ndani ikiwa ni kama sehemu ya kuongeza familia ya mitindo naushirikiano baina ya wabunifu wa bara na visiwani

Baadhi ya wabunifu watakaoshiriki ni Asia Idarous (Mshindi wa tuzo ya Humanitarian katika tuzo za SFW 2012), Dominick Godfrey, Subira Wahure, Ailinda Sawe, (Mshindi wa tuzo ya Origin Africa, SFW 2012), Martin Kadinda (Mbunifu Bora wa Nguo za Kiume, SFW 2012), Sarah Masenga (Mbunifu Bora Chipukizi, SFW 2011), Gabriel Mollel (Mbunifu Bora wa Mwaka na Mbunifu Mvumbuzi wa mwaka, SFW 2012), Subira Wahure, Jamila Vera Swai, Salim Ali, Ahmed Abdul pamoja na mshindi wa tuzo ya Mbunifu Anaechipukia wa SFW 2012, Lucky Creation.  

Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa ya tarehe 15 mwezi wa huu visiwani Zanzibar



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging