Google PlusRSS FeedEmail

KIGOMA ALL STARS KUSIFU TANZANIA



KUTOKANA na mazoea yaliyozoeleka kwa baadhi ya wasanii wa bongo fleva kuimba nyimbo za mapenzi na kuacha kuimba vitu vingine vikiwemo vya kusifia nchi hali hiyo imekuwa tofauti kwa wanamuziki wanaounda kundi la la Kigoma all Stars kwa kuimba nyimbo zinazosifia nchi

Hali hiyo imejitokeza baada ya kundi hilo kutoa nyimbo inayojulikana kwa jina la Leka Dutigite ikiwa inasifu mkoa wa kigoma na kuweza kufanya vizuri na sasa wameachia nyimbo nyingine inayoitwa Nyumbani inayosifu nchi ya Tanzania

Nyimbo hiyo inasifu Tanzania na rasilimali zilizomo pamoja na utajili uliopo katika nchi hii na kufurahia kuwa mtanzania

Akizungumza mmoja wa wasanii anayeunda kundi hilo Mwasiti Almasi alisema kuwa wameamua kufanya tofauti kwa ajili ya kuwa na mashabiki wa aina tofauti tofauti

Alisema nyimbo za bongo fleva zinamipaka na mashabiki wake wamegawanyika, hali hiyo imewapa changamoto ya kufikiria ni aina gani ya muziki utakao kuwa na mashabiki wote bila ya kuwagawa mashabiki

Mwasiti aliongezea kuwa nyimbo ya Nyumbani imezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo juu ya muungano wa nchi Tanzania na Zanzibar, rasilimali zilizopo kuutangaza utalii wa nchi pamoja na watanzania kujivunia kuwa watanzania

Muimbaji mwingine ambaye pia na yeye anaunda kundi hilo Chege alisema kuwa wameamua kuwa tofauti ili kuwavutia zaidi watanzania na kuweza kufikisha ujumbe

Alisema moja ya kazi kubwa ya msanii ni kuwa mbunifu hivyo hapo wametafuta ubunifu na kufikiria watoke kwa hali gani

Kundi la Kigoma Stars limeundwa na wanamuziki 15 wenye majina katika muziki wa bongo fleva baadhi ya wanamuziki hao ni Abdukiba, Baba Levo,Banana Zoro, Chege, Diamond, Mwasiti, Makomando, Ommy Dimpoz


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging