MSANII wa muziki wa bongo fleva Khalid Mohamed a.k.a Top In Dar, Tid aelezea nia yake ya kwenda kushiriki shindano la 'Big Brother Africa'(BBA) ni kutokana na baadhi ya Watanzania walio wengi kumuitaji akawawakilishe katika shindano hilo.
Akizungumza na Maisha Tid alisema kuwa watanzania ndio waliompendekeza kwa kumpigia kura na kufanikiwa kupata kura 600 kati ya 900 ili akawawakilishe kwenye shindano hilo.
Alisema kuwa anaingia kwenye shindano hilo ambapo mwaka huu linaitwa 'Big Brother Superstars' ambapo washiriki watakao shiriki ni wale wenye majina katika nchi walizotoka ndio pamoja na wasanii wa muziki, filamu na wengineo.
Kutokana na washiri kuwa ni watu maarufu hivyo Tid aliwataka washiriki wenzie kujipanga na watambue kuwa ,Tanzania kuna vipaji mbalimbali hivyo wakae teyari kwa kuona kipaji alichonacho na anaamini kuwa atakuwa kinara zaidi ya wenzake kwani sifa anazo
" Naamini nitafanya vizuri kwani Watanzania wenyewe ndio walionichagua na sasa kuna muamko naamini hata zoezi la kunipigia kura nalo litakuwa vizuri ingawa bado nawasisitiza kabla sijaingia mjengoni kuwa kura zao ndio zitakazo nipa ushindi wangu," alisema Tid
Baadhi ya mashabiki wameonekana kumuunga mkono msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Facebook na baadhi ya wengine wanaamini kuwa atawakilisha vyema katika mashindano hayo kwa sababu anavigezo vyote huku ucheshi ukimuweka katika nafasi nzuri ya kuweza kushinda.








