Jina kamili : Willow Camile Smith
Kazi anayofanya
Yeye ni muimbaji kutoka nchini Marekani
Mwaka aliozaliwa:
Amezaliwa oktoba 31 mwaka 2000
Ni mtoto wa nani ?
Ni mtoto wa mkongwe wa muziki na filamu Will Smith na Jada Pinkett Smith ambaye pia ni kama mume wake
Lini alianza kuonekana katika ulimwengu wa filamu ? :
Willow alianza kuonekana katika ulimwengu wa filamu mwaka 2007 alipoigiza 'Im Legend' na baadaye alionekana katika 'Kit Kitredge'
Tuzo alizopata?
Filamu hizo mbili zilimfanya apate tuzo ya kuwa msanii bora chipukizi kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha huku akiwa na umri mdogo
Lini alianza muziki?
Mwaka 2010 ndipo alijikita katika tasnia ya muziki baada ya kutoa 'single' yake ya kwanza 'Whip My Hair' na 21 Girl Century
Nyimbo hizo mbili zilimvutioa mtayarishaji mkongwe na muimbaji wa Hip Pop Jay Z ambapo alimpa mkataba katika studio ya Nation Roc
katika familia yao wako wangapi?
Willow anandugu zake wawili Trey Smith ambaye amechangia baba na Jade Smith
Mbali na muziki:
Willow na ndugu zake ni mabarozi vijana katika kwa ajili ya maradi wa Zambia ambayo unatoa msaada kwa watoto yatima wazazi wao walifariki kutokana na UKIMWI kwa kushirikiana na Hasbro
Wanamchakato gani ?
Kwa sasa Willow na ndugu yake wapo katika mchakato wa kutoa albamu mpya ya pamoja baada ya mama yao Jada kuthibitisha hilo
Wasanii wengi wa nchi zilizoendelea wamekuwa wakihakikisha vizazi vyao vinafuata mfano wa shughuli zao ambazo baadaye wanakuwa nyota na kutamba anga mbalimbali
Hii tumewahi kuwashuhudia wakali mbalimbali ambao watoto wao wakianza kupata akili huanza kuwafundisha fani mbalimbali iwe kwa upande wa wanamuziki, waigizaji au hata kwa wacheza mpira huakikisha kizazi chao kinafuata nyayo hizo katika siku za usoni