WANENGUAJI WA KIKE WAFUNGUKA
WANENGUAJI wa kike wawalalamikia baadhi ya mashabiki wao kitendo cha kuwatunza fedha na kuziweka sehemu za siri kitendo hicho ambacho wao wanakiona ni sehemu ya udharilishaji hususani kwenye kazi yao
Hayo yalizungumzwa na mnenguaji wa bendi ya Extra Bongo 'wazee wa kizigo' Sabrina Mathew ' Mayonaisi' wakati wa shoo yao inayofanyika kila mwisho wa wiki jijini Dar es Salaam
Alisema kuwa siyo ustaarabu kwa baadhi ya mashabiki wao kuwatunza fedha na kuziweka sehemu zao za siri wawapo stagen, kwani hali hiyo ni sawa na udharilishaji na wanajiona kukosewa heshima sehemu ya kazi yao
Alisema kuwa ustaarabu ni kuwatunza kwa heshima bila ya kujali ni nani unayemtunza kwani kwa kufanya hivyo mshabiki bado ataonyesha thamani nakujali muziki wa dansi Tanzania
"Unajua si ustarabu kuja kunishika sehemu zangu za siri na kuniwekee fedha wakati unaweza kunitunza mkononi au kuweka chini bado utaonekana mstaarabu na kuonyesha kuwa unajali muziki wa dansi nchini" alisema Mayonaisi
Pamoja na hayo Mayonaisi alielezea sababu zilizomfanya kuhama bendi ya Twanga Pepeta na kuhamia Extra Bongo kuwa kutafuta maslahi kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha pamoja na kimuziki
Kwa upande wake mnenguaji Nadi2ne Conpresor ambaye ni raia wa Kongo kwa sasa yupo kwenye bendi ya Extra Bongo alisema kuwa anashangazwa na mashabiki wanaofanya vitendo hivyo na kuwaomba kuwa wastaarabu na kuheshimu kazi yao







