Google PlusRSS FeedEmail

MIWANI YA ELTON JOHN YAZUA UTATA



KUTOKANA na kupenda kuvaa miwani kila wakati yenye mitindo tofauti mwanamuziki wa Uingereza Elton John ameomba kuwekewa chumba cha ziada kwa ajili ya kuhifadhia miwani yake nchini Brazil ambapo atakuwa kwenye ziara ya muziki nchini humo

Mwanamuziki huyo atafanya ziara nchini humo, huku akitarajiwa kufanya shoo nne mfurulizo ikiwa ni sehemu moja ya kuadhimisha miaka 40 ya albamu yake iliyopewa jina la 'Rocket Man'

Kwa mujibu wa gazeti la Brazil,nyota huyo awewaagiza waandaaji wa ziara hiyo kumwaandalia chumba cha ziada kwa ajili ya kuhifadhia miwani yake, kwani ni sehemu ya maisha yake

Pamoja na kuagiza kuandaliwa chumba hicho pia muimbaji huyo ameweka bayana kuwa chumba hicho kinatakiwa kiwe na joto lisilopungua wala kuongezeka nyuzi joto 16,na ili kuongeza mvuto na kufanya chumba hicho kiwe cha kipekee lazima kipambwe na mauwa waridi yenye manukato mazuri

"Anaamini kuwa anamahitaji mengi hususani katika kukamilisha uvaaji wake anahitaji zaidi chumba chake cha kubadilisha nguo kiwe na maua waridi yenye rangi nyekundu 16 pamoja na maua meupe "aliongezea Elton John

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging