WATANZANIA MAARUFU KWENYE MTANDAO WA TWITTER
MITANDAO ya kijamii imeendelea kuchukua nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kwa kupitia fursa mbalimbali zinazotumiwa na makundi ya watu kusambaza taarifa mitandaoni hususani watu wenye majina makubwa
Kutokana na kile wanachokiandika na kutuma kwenye mtandao hususani wa 'Twitter'kila wakati baadhi ya watu mashuhuri hujikuta wakiwashawishi watu kuwafwatilia katika mtandao yao na ndiyo sababu inayosababisha watu hao kuwa na watu wengi wanaowafuatilia kwenye mtandao huo.
Wafuatao ni baadhi ya watu mashuhuri Tanzania ambao wanaongoza kwa kuwa na wafuatiliaji wengi pamoja na kutuma jumbe (post) nyingi kila wakati
Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameongoza kwa kuwa na wafuasi wapatao 52,126 huku akiwa ametuma jumbe 'tweets' 1,375
Zitto Kabwe
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini amejikuta akizidi kujiongezea umaarufu kwa kuwa na wafuasi 42,802 huku akionekana akiwa 'tweets' 13,422
Kutokana na idadi ya watu wanaowafatilia Rais Kikwete na Zitto utagundua kuwa rais ameongoza kwa kuwa na wafuasi wengi ingawa Zitto amevunja rekodi kwa kuweka 'tweets' nyingi zaidi ya Kikwete
Flavian Matata
Miss Universe Tanzania mwaka 2007-2008 ambaye sasa ni mwanamitindo wa kimataifa ameshika nafasi ya tatu kwa kuwa na wafuasi wapatao 37,050 ambapo ameshatuma 'tweets' 29,655
Ambwene Yesaya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amevusha muziki nje ya Tanzania, msanii huyo ana wafuasi wapatao 36,280 ameweza kuwa karibu na wafuasi wake kwa kutuma 'tweets' 19,385
Millard Ayo
Ni mtangazaji wa Kituo cha Redio Clouds Fm amezidi kujiongezea umaarufu kwa kutumia nafasi yake kuelimisha jamii pamoja na kuhabarisha kwa kuwa na wafuasi 34,124,pamoja na 'tweets' 20358
Mwana Fa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Hip Hop anawafuasi wapatao 29,540
January Makamba
Naibu waziri wa Sayansi Technolgy na Mawasiliano ambapo pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli naye pia ameweza kufikisha idadi ya wafuasi wapatao 26,734 huku akiwa ameweza kuweka ukaribu na wafuasi wake kwa kutuma 'tweets' zipatao 7244
Profesa Jay
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya anawafuasi 22,288 huku akiwa ametuma 'tweets'13,017
Salama Jabili
Huyu ni mtangazaji wa kipindi cha mkasi kinachorushwa katika televisheni ya East Afrika anawafuasi 20,941 ametuma 'tweets' 37,701
Halma Mdee
Mbunge wa jimbo la Kawe kupitia tiketi ya CHADEMA ameweza kuwa na wafuasi wapatao 12462
Hao ni baadhi ya watu maarufu Tanzania ambao wanatumia mtandao wa Twitter kwa ajili ya kupashana habari pamoja na kuelimisha jamii