NGISAH ANAJIVUNIA KUWA KIBONGE
Muigizaji Roselyn Ngissah amesema haoni shida kuwa na mwili mkubwa na wala hafikirii kufanya uchaguzi wa wa vyakula, ambapo aliweza kuingia kwenye tasnia hiyo akiwa na mwili mkubwa hivyo hali hiyo haiwezi kumzuia kutimiza malengo yake
Alisema kuwa watu wengi walisema hawezi kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo kutokana na kuwa na mwili mkubwa lakini aliwadhihirishia kuwa hizo ni mbwembwe tu kwani kipaji ndio kila kitu
Alifafanua kuwa wakati alianza kuigiza waandaaji wengi walimtaka apunguze mwili ili aweze kucheza kwenye nafasi mbalimbali lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu nafurahia jinsi alivyo