RIHANAA KAMA MICHAEL JACKSON
Mwanamuziki nyota Rihanna amewaacha hoi mashabiki wake, baada ya kuibuka na mtindo wa uchezaji ambao alikuwa akitumia mfalme wa Pop Michael Jackson
Rihanna alifanya kituko hicho juzi wakati wa onesho lake alilolifanya mjini Los Angels nchini Marekani, hata hivyo inaelezwa kuwa siyo mwanamuziki wa kwanza wa kike kuiga uchezaji huo wa kushika sehemu za siri
Miongoni mwa wasanii wa kike wanaotajwa kucheza kwa staili hiyo ni Madonna ambaye alifanya hivyo kwenye maonyesho yake hivi karibuni








