Kesi ya kuomba talaka iliyofunguliwa na muigizaji na muandaaji wa vipindi vya televisheni Kim Kardashian dhidi ya mumewe Kris Humphriess inatarajiwa kuendeshwa kifamilia
Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama timu ya wanasheria wa mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 32,inatarajia kuwaita mama yake mzazi na meneja wake Kris Jenner kuwa mashuhuda kwenye kesi hiyo
Taarifa hizo za nyaraka za Mahakama zinaeleza kuwa wanasheria ndio watajadiliana kuhusu kesi hiyo lakini dada zake nyota huyo Khloe na Kourtney hawatahudhuria kesi hiyo








