NEY APANDA JUKWAANI AKIWA NA VIATU TOFAUTI
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego avaa viatu viwili tofauti katika uzinduzi wa video ya nyimbo inayojulikana 'Muziki Gani' aliyoimba kwa kushirikiana na msanii mwenzie Diamond .
Ney wa Mitego alipanda jukwaani akiwa amevaa viatu vya aina ya tofauti huku akionyesha hali ya kutokuwa na wasiwasi wa kile alichokifanya sababu iliyoibua maswali mengi kwa mashabiki wake
Akizungumza baada ya shoo hiyo Ney alisema kuwa ameamua kuvaa viatu tofauti ili kujitofautisha na wasanii wengine wa Hip Hop na awe na mtindo wa aina yake mwenyewe







