Google PlusRSS FeedEmail

NGWAIR AFARIKI DUNIA



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Albert Mangwea 'Ngwair' amefariki dunia leo akiwa  Afrika ya Kusini ambapo alikwenda kufanya shoo maalum nchini humo.

Taalifa  zilizopatikana hivi punde  zinaeleza Ngair amefariki dunia katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini Johannesburg nchini humo, ingawa sababu za kifo chake bado hazijapatikana.

Taarifa hizo zilieleza kuwa msanii huyo alikuwa nchini humo kwa mualiko wa kufanya shoo ambapo jana ndio ilikuwa siku yake ya kurudi jijini Dar es Salaam.

Ngwair alikuwa ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alikuwa anaimba miondoko ya Hip Hop kutoka 'East Zoo' ambapo ameweza kufanya kazi kwa kushirikiana na  baadhi ya wasanii wenzie  aliwemo Jay Mo, nyimbo inayojulika kwa jina la 'Kimyakimya'.

Msanii huyo pia amewahi kufanya kazi katika lebo mbalimbali za muziki ikiwemo ya Zizzou Entertainment

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging