Nchi zingine zilizoko katika hatari ya kukosa washiriki kwenye jumba hilo ni pamoja na Kenya ambayo imebakiwa na mshiriki mmoja ambaye anaitwa Annabel na Afrika Kusini ambayo nayo jana ilipoteza mshiriki mmoja ambaye ni Koketso na kubakiwa na Angelo pekee.
Kwa upande wa Tanzania mshiriki wetu Feza ambaye alikuwa kikaangoni alipona baada ya kura zake kutosha kumbakisha katika jumba hilo baada ya Betty aliyekuwa HOH kumtoa mpenzi wake Bolt katika kikaango na kumuingiza Feza. Shindano hilo linaendelea kwa washiriki kupendekeza tena washiriki ambao wangependa waingie katika kikaango kabla ya kupigiwa kura na watazamaji mshiriki ambaye wanaona anafaa kubakia ndani ya mjengo huo.










