BIEBER AENDELEZA BANGI
Baada ya mashabiki wake kujiuliza maswali mengi juu ya mwenendo mzima wa tabia ya msanii kinda wa Pop Justin Bieber, ameendelea kudhihirisha kuwa ni mpenzi wa kuvuta bangi baada ya kuonekana katika picha na msokoto huo.
Bieber aliamua kutuma picha hiyo ikimuonesha na misokoto ya dawa hiyo ya kulevya katika mtandao wa instagram.








