Google PlusRSS FeedEmail

BIG BROTHER AFRIKA, THE CHASE: WASHIRIKI WABADILISHANA NYUMBA.

SHINDANO la Big Brother Afrika, The Chase lilikiwa limefikia siku yake ya tano washiriki wameendelea na shughuli zao za hapa na pale wanazopewa na BIGGIE huku watanzania FEZA KESSY ambaye anamalizia muda wake wa kuwa kiranja ndani jumba hilo na AMY NANDO wakionekana kuendelea vyema. Washiriki hao wako salama katika wiki hii ya kwanza ya kupigiwa kura za kutoka ndani ya jumba hilo. 
Ikiwa imebaki siku moja kabla ya siku ya washiriki wawili wa kwanza kati ya watano waliopo katika Danger Zone ambao watapata kura chache kutolewa BIGGIE amekuja na wazo la kubadilisha baadhi ya washiriki kutoka katika nyumba mbili za DIAMOND na RUBY. Katika Arena, BIGGIE aliandaa shindano kati ya nyumba hizo mbili na nyumba itakayoshinda washiriki wake wawili watabadilishana na wengine wawili kutoka katika nyumba nyingine. Na kiranja wa nyumba au HEAD OF THE HOUSE (HOH) ndio atachagua watu hao katika chumba cha mazungumzo DIARY ROOM.  
Baada ya uamuzi wa HOH washiriki waliochaguliwa watapewa dakika 30 kujiandaa na kuondoka kwenda katika nyumba nyingine na pia katika zoezi hilo ilifafanuliwa kuwa washiriki watakaobadilishana kama wapo katika Danger Zone watabakia hivyohivyo na kama hapana au walipona watapata kinga katika uchaguzi unaokuja (Nominations). Katika jumba la Diamond FEZA akiwa kama HOH mara ya kwanza aliwachagua Denzel na Betty lakini baada ya kufikiria sana alimtoa Betty na kumuweka Neyll wakati Beverly ambaye ni HOH wa Ruby yeye aliwachagua Hakeem na Melvin. Kwa maana hiyo Denzel na Neyll watahamia jumba la Ruby wakati Hakeem na Melvin watakwenda jumba la Diamond.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging