Google PlusRSS FeedEmail

BINTI WA MICHAEL JACKSON ALAZWA BAADA YA KUJARIBU KUJIUA

Binti wa Michael Jackson, Paris, alikimbizwa hospitali Jumatano alfajiri baada ya kilichotajwa kuwa ni kujaribu kujiua, kwa mujibu wa website ya TMZ. Msemaji wa polisi amesema polisi waliharakisha kwenye nyumba anayoishi Paris Jackon, jijini Los Angeles kwa ajili ya “medical situation.” Msemaji wa polisi alikataa kutaja mhusika.
Paris aliandika tweets zinazoonyesha alikua katika hali ya huzuni Jumanne usiku kama: ““yesterday, all my troubles seemed so far away now it looks as though they’re here to stay” na “i wonder why tears are salty?” TMZ wamesema chanzo chao kwamba Paris alijaribu kujiua, na kuongeza aliondolewa nyumbani kwa machela baada ya mtu mwingine nyumbani hapo kupiga simu na kuripoti “drug overdose.”

Chanzo kilichokua karibu na familia ya Jackson kimesema Paris alikua na mikato kadhaa kwenye mikono. Chanzo hicho kiliongeza kuwa hii sio mara ya kwanza kwa binti huyo kujaribu kujiua, lakini safari hii ilikua serious zaidi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging