Baada ya ukimya wa muda mfupi msanii wa miondoko ya Hip Hop Gosby ametoa nafasi kwa wasichana watatu watakaoweza kujibu maswali yanayohusu muziki wake kwa ufasaha kwenda kusikiliza kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya alioupa jina la 'Baby Making Swag aka BMS' siku ya Jumatano (leo) kwenye studio za B'Hits zilizopo Kawe.
Aliweka wazi kuwa ameamua kuwachagua wasichana pekee yake kwa sababu mahadhi na ujumbe unaopatikana kwenye nyimbo hiyo unawagusa wasichana zaidi.
Mbali na hilo pia ameamua kuwafanya wasikilizaji wake kuwa wa kwanza kuusikiliza muziki huo, huku akitarajia kupata ushauri kupitia mashabiki wake.








