Google PlusRSS FeedEmail

KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2013 LIVE ON LIVESTREAM

Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music
Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni
8. Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio
lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa
Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu
watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la
Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu
wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini. Pia
tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja
kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za
Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application
ya LIVESTREAM itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao
wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013 na katika Blogs mbalimbali.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging