Google PlusRSS FeedEmail

KIM KARDASHIANA KUFUNGA NDOA NA KANYE WEST


KITENDO cha Kim Kardashian kupata mtoto wa kike, huku mtoto huyo amepewa jina la North huenda kimemvutia zaidi mchumba wake Kanye West na kuamua kutangaza ndoa ambayo itafungwa hivi karibuni.

Kanye ameamua kutangaza  rasmi ndoa yake na mwanadada Kim Kardashian ingawa hajamvalisha pete ya uchumba.

Hatua ya Kanye kutangaza ndoa ya mama wa mtoto imekuja siku chache baada ya ndoa ya Kim na aliyekuwa mume wake Kris Humphries kufikia tamati rasmi kisheria wiki iliyopita baada ya mvutano wa muda mrefu na Kris waliyekaa kwenye ndoa kwa siku 72 kabla ya Kim hajaomba talaka Octeber 2011.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun inadaiwa kuwa mastaa hao wanategemea kufunga ndoa yao mwezi September mwaka huu jijini Paris, Ufaransa

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging