ANGELINA JOLIE ATAJWA KULIPWA PESA NYINGI DUNIANI
Ingawa hajatoa filamu tangu mwaka 2010 iliyokuwa inajulikana kwa jina la 'The Tourist' muigizaji wa kimataifa Angelina Jolie ametajwa kuwa mwigizaji wa kike anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani.
Jolie ametajwa na mtandao wa Forbes kupitia ripoti yake kuwa katika kipindi cha mwezi June mwaka jana na june mwaka huu ameingiza kiasi cha dola milioni 33 ambazo ni zaidi ya sh. bilioni 48 za kitanzania.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa Jolie amekusanya mkwanja kutokana na mkataba wa kushiriki katika filamu mpya 'Maleficent' iliyolipwa dola milioni 15 na inatarajia kutoka mwakani , huku akiwa ameingiza dola milioni 10 akiwa kama balozi wa brand maarufu