CHIKA AONJA JOTO YA JIWE
NYOTA wa filamu nchini hapa, Chika Ike ameonja joto ya jiwe baada ya maisha ya ndoa kumkataa.
Ike ameamua kufunguka baada ya kubanwa na waandishi kwanini amekimbia ndoa yake na kurejea kuwa ‘single girl’.“Sikuwahi hata siku moja kufurahia maisha ya ndoa nikaona heri nibwage manyanga.
“Ukweli ni kuwa kuna wakati unakutwa na jambo linalokulazimu uachane nalo ili usiendelee kuteseka na gunia la misumari kichwani,” alisema. Aliongeza kuwa ndoa nyingi zipo zipo tu na kwamba wanandoa wengi hujilazimisha kuwamo katika kundi hilo ili kutowaudhi wazazi au marafiki.
“Furaha ndio kila kitu. Maisha ya kubanana mimi sitaki tena. Nataka kuwa huru na mambo yangu.”








