MSANII nyota wa muziki nchini Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ anatarajia kuvamia Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kwenda kuitambulisha albamu yake mpya ya Nothing But The Trust siku ya Iddi El Fitr.
Katika ziara hiyo Jay Dee anatarajia kwenda na bendi yake ya Machozi huku akisindikizwa na Profesa Jay katika maonyesho yatakayofanyika sehemu mbili tofauti.
Akizungumza Dar es Salaam, Meneja wa Jay Dee, Gadna G Habash ‘Captain’ alisema kuwa ziara ya kwenda ni mkakati uliokuwepo kwa muda mrefu kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wao wa mikoani nakuwapelekea albamu mpya ya Nothing But The Trust iliyotoka hivi karibuni wakati wa kutimiza miaka 13 ya msanii huyo .
Alisema kuwa onyesho la kwanza linatarajiwa kufanyika Iddi Mosi katika Ukumbi wa Triple A ambapo mashabiki watapata nafasi ya kusikiliza nyimbo mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za zamani na mpya.
Alisema kuwa baada ya onyesho hilo la Iddi Mosi, Iddi Pili wanatarajia kufanya onyesho la aina yake Botanical Garden kwa ajili ya kuburudisha watoto pamoja na familia zao.
Alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na mashabiki wa Jay Dee wa Arusha watapata burudani ya aina yake kutoka kwa Machozi Band wakiambatana na Profesa Jay.
Alisema kuwa hata hivyo Jay Dee hajafanya ziara mikoani kwa kipindi kirefu na hiyo ndio itakuwa nafasi muhimu ya kukata kiu na mashabiki wake wa mikoani.
“Tunatarajia kufanya ziara ya aina yake Mkoani Arusha kwa ajili ya kuipeleka albamu mpya na pia Jay Dee hajafanya ziara mikoani kwa muda mrefu, hii ndio itakuwa fursa pekee kwa mashabiki wake baada ya kumaliza Arusha tunatarajia kwenda katika mikoa mingine” alisema.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.