LAURYN HILL AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO GEREZANI
Mwimbaji Lauryn Hill ambaye amewahi kutwaa tuzo za muziki wa grammy ameanza kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani alichohukumiwa baada ya kupatikana na kosa la kukwepa kodi kiasi cha dola za marekani milioni moja sawa na paundi 670,000 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Hill anatumikia kifungo hicho katika gereza la Danbury lililopo katika jimbo la Connecticut, alisema Ed Ross, msemaji wa gereza hilo.