Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzoa alisema kuwa, wadada hao wanatarajia kupanda kizimbani tena Septamba 13 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili Aliweka wazi kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea katika nchi zote mbili, na bado wasichana hao wanashikiliwa na jeshi la polisi la nchini humo.
"Upelelezi unaendelea huku kila nchi ikitegemeana kwa ajili ya uchunguzi huo pamoja na kupashana habari tunapofikia na wao wanapofikia" alisema Nzoa.
Masogange na mwenzie walikamatwa Julai 5 mwaka huu wakiwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya ambazo zinajulikana kwa jina la 'Kemikali bashilifu'