Google PlusRSS FeedEmail

KITIME AWACHAMBUA WANAMUZIKI WAKONGWE


MWANAMUZIKI wa bendi kongwe nchini ya The Kilimanjaro 'Wananjenje', John Kitime afichua sababu za baadhi ya wanamuziki kustaafu muziki huku wakiwa na hali duni kiuchumi.

Hali hiyo imekuja baada ya mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini wa bendi ya Msondo Ngoma, Muhidini Gurumo kutangaza kustaafu muziki akiwa na umri wa miaka 73, huku akiwa na hali mbaya ya kuichumi .

Akizungumza na jarida hili jijini Dar es Salaam, Kitime aliweka wazi kuwa wanamuziki wakongwe kustaafu muziki ikiwa hali zao kiuchumi kuwa mbaya, hiyo inaonesha hali halisi ya maisha ya kitanzania.

Alisema wapo baadhi ya wanamuziki wengi wakongwe, wameacha muziki na maisha yao yapo duni ingawa waliutumikia muziki huo kwa kipindi kirefu.

Kitime alisema si tu wanamuziki, bali hayo ni maisha halisi ya Watanzania hata kwa baadhi ya viongozi waliostaafu maisha yao yapo duni.

"Kutokana na hali hiyo, vijana sasa wanalazimika kuingia ofisini na kuwa mafisadi ili waweze kujikimu kimaisha kwani wanafahamu akizeeka hali inakuwa mbaya zaidi ya hapo," alisema Kitime.

Aliongezea kuwa Gurumo, ndiye anaonesha hali halisi ya wazee wa Kitanzania ilivyo kwani yeye ni kioo cha jamii.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging