Msanii huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa single inayoenda kwa jina la 'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku hiyo ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.
Akizungumza na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya shoo hiyo, Rose aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na kazi ya filamu ambayo ameizoea.
Alisema upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi kukosea tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata nafasi ya kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.
"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema Ndauka.
Aliongezea kuwa anamshukuru mtayarishaji wa muziki P Funk kwa kuweza kutambua kipaji chake hicho cha uimbaji na kuweza kumpa nafasi ya kushiriki katika nyimbo hiyo.
Kundi la hilo linaundwa na wasanii wawili akiwemo Chiwaman pamoja na 'Latino Man', ambapo wameachia single yao ikiambata na uzinduzi .