Google PlusRSS FeedEmail

RAY C AJIANDAA KURUDI KWENYE GEMU LA MUZIKI


BAADA ya ukimya mrefu na maswali kutoka kwa mashabiki  kupitia mtandao wa Instagram mwanadada
Rehema Chalamila 'Ray C' a.k.a Kiuno bila mfupa kuonekana hadharani tena, huku akifanya maandalizi ya
kurekodi nyimbo mbili mfululizo.

Mwanadada huyo ambaye anatarajia kurudi kwa kishindo huku akiwatisha wasanii ambao wapo kwenye gemu hilo kukaa sawa, amesema ameshaanza mandalizi ya kuandika baadhi ya nyimbo na teyari amejipanga kwa ajili ya kuingia studio.

Akizungumza katika moja ya mahojiano jijini Dar es Salaam Ray C, ameweka wazi kuwa ametambua kuwa mashabiki wake wanahitaji zaidi kusikiliza nyimbo zinazohusu maisha na siyo mapenzi sana ingawa ndio nyimbo alizozoea kuimba.

"Nafikiria kuimba zaidi maisha, kwani ni wakati jamii inatakiwa kujifunza na kusikiliza vitu vinavyohusu maisha ingawa tangu naanza kuimba nilikuwa naimba masuala ya mapenzi sana" alisema Ray C.

Alisema kuwa kila kitu kitaanza wiki hii ingawa kuandika nyimbo alishaanza muda kidogo na teyari zimekamilika baadhi ya nyimbo. Aliendelea kuweka wazi kuwa kutokana na kuonekana kuwa kibonge amejipanga kuanza kufanya mazoezi ili kupunguza mwili huo na kujiweka katika hali nzuri ya kumiliki stage.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging