Google PlusRSS FeedEmail

KESI YA JAYDEE YAPIGWA 'DANADANA ' TENA


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeahirisha tena kesi inayomkabiki msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 6 mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani leo ilipelekwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na Hakimu anayeshikiria kesihiyo Nyamlani kupata dharula, na kushindwa kuisikiliza kesi hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mume wa msanii huyo anayekabiliwa na kesi hiyo Gadna G. Habashi alidai kuwa walifika mahakamani hapo asubuhi na ndipo walipopata taarifa kuwa Hakimu huyo amepata dharula.

"Hakimu amepata dharula hivyo kesi yetu imesogezwa tena mbele hadi tarehe 6 mwezi huu ndipo itasikilizwa" alisema Gadna.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.

Kwa mujibu wa mdai huyo ambaye ni uongozi wa Clouds Media, ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blog yake.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging