MATUMIZI ya dawa za kulevya ni miongoni mwa vitu vinavyopingwa duniani kote, huku kila nchi ikiweka adhabu mbalimbali juu ya dawa hizo ili kuthibiti matumizi hayo.
Vita hiyo ambayo kila nchi imeweka mikakati yake ya jinsi ya kuthibiti matumizi hayo, huku nchi ya Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo inapigana na matumizi hayo ya dawa za kulevya.
Baadhi ya vijana wengi nchini wamekuwa wakijihusisha na matumizi hayo ya dawa za kulevya ikiwemo kutumia au kujihusisha kwenye biashara hiyo.
Hivi karibuni kumekuwa na ukamatwaji wa baadhi ya vijana wanaojihusisha na usafirishaji wa dawa hizo nje ya nchi wakiwa wanasafirisha dawa hizo.
Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya watanzania 254 wamekamatwa ughaibuni wakiwa wanasafirisha dawa za kulevya huku baadhi yao wakiwa wanatumikia kifungo nje ya nchi.
Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti kukamatwa kwa wasichana wawili akiwemo msanii wa muziki wa bongo fleva Agnes Masongange nchini Afrika Kusini wakisafirisha dawa za kutengenezea dawa za kulevya.
Kukamatwa kwa vijana hao inawezekana bado ikawa si tatizo nchini kwani 'mapapa' wale wahusika wenyewe wanaowatumia vijana hao wameshindwa kufikiwa na mkono wa sheria hali ambayo inasababisha tatizo hilo kuendelea kuwa kubwa.
Mbali na kukamatwa kwa vijana wanaotumika kusafirisha dawa hizo, kumekuwa na wimbi la baadhi ya wasanii kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya huku baadhi yao wakiona sifa kutumia dawa hizo.
Rehema Chalamila 'Ray C' ni miongoni mwa wasanii aliyekuwa akitumia dawa hizo hali iliyopelekea kushuka kiwango cha kisanaa na kushindwa kujiendeleza kimaisha.
Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wakike wachache waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya nchini ambaye alikuwa akitamba na nyimbo za mapenzi.
Ray C ni miongoni mwa wasanii wachache waliokiri kwa jamii kutumia dawa za kulevya ingawa wapo baadhi ya wasanii wanaotumia dawa hizo na hawajawahi kuthubutu kukirii kutumia dawa hizo.
Msanii huyo baada ya kujigundua kuwa amepoteza dira kwa kutumia dawa hizo za kulevya huku hela zake zote alizokuwa akipata kutokana na kazi yake ya muziki zilikuwa zikiishia katika manunuzi ya dawa hizo aliweza kuchukua hatua ya kujitoa kwenye tatizo hilo.
Msanii huyo aliweza kujigundua na kuchukua hatua, ingawa alishindwa kulitatua tatizo hilo pekee yake aliweza kupata msaada kutoka kwa familia yake na baadhi ya watu wanaomzunguka.
Kujitambua na kugundua alichokuwa akifanya si sahihi ni jambo la msingi ambalo baadhi ya wasanii wanaotumia dawa hizo wanatakiwa kuiga mfano huo ili kujiokoa katika matumizi hayo ambayo yanapelekea kuwapotezea dira katika maisha yao.
Ray C ni msanii ambaye ni mfano wa kuigwa kutokana na hatua kubwa aliyoamua kuichukua baada ya kujitambua na kuthamini thamani yake.
Wapo baadhi ya wasanii ambao wanatumia dawa hizo bila ya kujua ni sababu gani inayowapelekea kutumia dawa hizo, hali inayopelekea kushindwa kutoka katika matumizi ya dawa hizo.
Kutambua sababu pia ni moja ya njia ya kumtoa msanii huyo katika matumizi hayo na siyo kumshauri msanii kuacha kutumia dawa hizo bila ya kuanza kumjenga ili aweze kujitambua na kutambua thamani yake kwa jamii yake.
Hivi sasa baadhi ya wasanii wengi wamejiingiza katika matumizi ya dawa hizo na pindi wanapoulizwa nini chanjo cha wao kujiingiza katika hali hiyo, huwa majibu yao ni hali ngumu ya muziki, ikiwemo kukosa nafasi katika baadhi ya redio nyimbo zao kusikika, ndio chanjo cha wao kujihusisha na matumizi hayo.
Kama hiyo ni sababu msanii amejipanga vipi kukabiliana na sababu hiyo? kwa nini usijipange kwa kutumia njia nyingine ya kuutangaza muziki wako bila hata ya kutegemea redio yoyote nchini.
Baadhi ya wasanii wengi wanadhana ambayo imejijenga kuwa nyimbo yao isipopigwa kwenye redio fulani basi hawezi kusikika, mazoea hayo yamepelekea nyimbo ya msanii isipopigwa redio fulani msanii anakosa kujiamini na kuhisi teyari ameshakosa soko la muziki.
Kwa mtazamo wa kawaida msanii anaweza kutumia mitandao ya kijamii ili kuweza kuzitangaza nyimbo zake zaidi kuliko kuitegemea hiyo redio ambayo wawo wanahisi bila hiyo hawawezi kusikika.
Acheni kuitupia lawama redio hiyo, wasanii mnatakiwa kujipanga ili kukabiliana na ushindani mkubwa katika tasnia hii ya muziki.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.