MSANII wa filamu nchini Single Mtambalike 'Richi Richi' amekuwa kivuto katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age uliofanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baada ya kupanda jukwaani na 'kummwagia' kitita cha fedha msanii mwenzake Elizabety Michael 'Lulu'.
Richi alijikuta akivutiwa na msanii Lulu mara baada ya kuimba kibao cha Yahaya kilichoimbwa na muimbaji Lady Jaydee, mara baada ya kumaliza kuizindua movi yake hiyo ambapo alitoa fursa kwa mashabiki wake waliohudhuria uzinduzi huo kuiangalia kwa dakika 10.
Richi alishindwa kuvumilia mara baada ya kusikia msanii huyo anaimba nyimbo ambayo kwa upande wake inamvutia, hali iliyopelekea kupanda jukwaani na kumwagia kitita cha fedha huku akionyesha kuifurahia
nyimbo hiyo.
Lulu akiokota fedha anazotunzwa na Richi Richi, huku msanii huyo anaonekana akiendelea kmrushia fedha
Msanii Richi akimtunza fedha Lulu mara baada ya kuimba nyimbo ya Yahaya iliyoimbwa na msanii Lady Jaydee
Msanii JB akifurahia mara baada ya msanii mwenzake Rich Rich alipomaliza kumtunza Lulu jukwaani.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.







