MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnumz ni miongoni wahanga katika ajari ya moto iliyotokea katika Uwanja wa Ndege nchini Kenya.
Moto huo umetokea majira ya saa moja asubuhi ndani ya jiji hilo la Nairobi ambapo msanii huyo alikuwa amewasili uwanjani hapo kutokea nchini Afrika Kusini alipoenda kwa ajili ya kujiendeleza na masomo yake ingawa haijafahamika ni masomo gani ambayo ameenda kusomea nchini humo.
"Nilikuwa napita kubadilisha ndege kurejea nyumbani Bongo Lakini maswahibu haya yaliyotokea majira ya saa 1 asubuhi huku mimi na abiria wengine tukisubiri kwenye ndege ghafla tulikuja kujuzwa kuwa hali ya usalama pale Airport haikuwa shwari na tulivyotoka kwenye ndege
ndio niliposhudia uwanja wa ndege wa Kenya ukiwaka moto…" hicho ndicho alichoandika kupitia mtandao wake.
Kutokana na hali hiyo imepelekea yeye na abiria kukwama kusafiri ambapo leo msanii huyo alikuwa akitarajia kufika nchini Tanzania.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.