MSANII wa muziki wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop Gwamaka Kaihula 'King Crazy Gk', amerudi kwenye gemu la muziki huo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, huku akiweka wazi kuwa kundi la TMK wanaume walitambue kundi la East Coast kuwa ndio walimu wao.
Gk katika ujio wake huo ameweza kuachia wimbo wake unaojulikana kwa jina la 'Baraka au Laana', ulioambatana na video ya wimbo huo, huku akiwa ni miongoni mwa wasanii waliotokea katika kundi la East Coast.
Akizungumza katika kipindi cha Xxl kinachorushwa na Clouds Fm wakati akiutambulisha wimbo huo Gk aliweka wazi kuwa anaamini ushindani wa muziki uliokuwa kipindi hiko ingawa siku zote wao kama kundi hilo ndio waliokuwa waalimu wa muziki kwa baadhi ya wasanii wenzao.
Gk aliweka wazi kuwa kundi hilo liliweza kuwafundisha baadhi ya wasanii akiwemo Juma Nature kuufanya muziki wake kuonekana wa tofauti, hivyo katika hali yakawaida anaamini kuwa kundi la East Coast ni moja ya kundi lililoibuwa wasanii wengi ambao sasa wanamajina katika tasnia hiyo.
Msanii huyo alisema kuwa ujio wake umekuja tofauti kutokana na hali halisi ya muziki kwa kipindi hiki ambapo mashabiki wanataka kusikia ukweli wa vitu vinavyowazunguka na si masuala ya mapenzi kama ilivyozoeleka.








