BARNABA AWA MLEZI BORA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Barnaba Elias ameonekana kuwa ni baba bora baada ya kutumia muda wake kwa ajili ya malezi ya mtoto wake wa kiume anayejulikana kwa jina la Steve.
Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka video inayomuonesha akimuimbia mtoto wake huku akiwa anapiga gitaa wote wakionekana wakiwa na furaha.
Akizungumza na jarida hili Barnaba aliweka wazi kuwa huwa anatumia muda wake mwingi wa mapumziko kukaa na familia yake hususani mtoto wake anayekuwa naye mbali kipindi ambacho yupo katika shughuri za kikazi.
Alisema moja ya maisha yake ni kukaa na mtoto huyo ili aweze kumpa mapenzi yanayostahili kama mzazi anayejali familia yake.
"Mimi nampenda sana mwanangu na kipindi chote cha mapumziko huwa ninakaa na mwanangu ili niweze kumpa mapenzi ambayo naamini anayafurahia kwa namna mmoja au nyingine na kupata kufahamu kuwa mimi ni baba bora kwake" alisema Barnaba boy.