Mwanamuziki Britney Spears amepata bonge la dili nchini Marekani ambapo atakuwa akilipwa dola 310,000 kwa shoo moja ambazo ni zaidi ya dola milioni 15 kwa mwaka.
Hata hivyo dau hilo haliwezi kufikia fedha ambazo anapata mwanamuziki Celine Dion, mkataba wa msanii huyo utakuwa ni wa miaka miwili ambapo atakuwa akitumbuiza kwenye ukumbi wa Planet Hollywood, kwa mujibu wa mkataba huo muimbaji huyo atapokea kitita cha dola za kimarekani 310, 000 kwa kila shoo atakayokuwa akiifanya.