Msanii huyo aliamua kuvua nguo na kutembea uchi hotelini hapo ingawa sababu za kufanya hivyo hazijajulikana bado. Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti video inayomuonesha msanii huyo akiwa hotelini hapo akiwa amevaa boxer na alipofika kwenye kona ya korido alivua boxer hiyo na kuanza kukimbia akiwa uchi kuelekea kuelekea upande mwingine.
Video hiyo ilionesha baada ya sekunde chache alipita muhudumu wa hoteli hiyo, ndipo DMX alionekana tena akirudi kwa kukimbia hadi pale alipoivua boxer yake na kuamua kuivaa tena.
Baada ya kuivaa nguo hiyo aliamua kuruda alipotokea mwanzo kwa mwendo wa kawaida, huku akionyesha hana wasiwasi wowote kwa kitu alichokifanya.
DMX alipoulizwa na mtandao wa TMZ juu ya kuamua kutembea uchi hotelini hapo alidai kuwa alijisikia tu
kufanya alichokifanya na hana majuto yoyote juu ya kitendo hicho.