Hali hiyo imekuja baada ya Hafsa kuibuka na kuamua kumuenzi muimbaji huyo kwa kuimba nyimbo hiyo ambayo imetungwa na Muhidi Gurumo.
Nyimbo hiyo ilipata umaarufu ukiwa chini ya Nuta Jazz Band uitwao 'Nimuokoe Nani' ambao ulitungwa na Gurumo, ambapo msanii huyo wa zouk ameamua kuurudia kurekodi upya wimbo huo ikiwa ishara ya kumuenzi msanii huyo.
"Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyia mtihani wa kuuimba wote wimbo huyo ambapo alilidhika na uimbaji wangu ndipo alipoweza kuniruhusu kwenda kurekodi" alisema Hafsa.
Msanii huyo anayetamba na wimbo wa 'Presha' aliomshirikisha Banana Zorro ameweka wazi kuwa ameamaua kumuenzi muimbaji huyo kwani kipindi ambacho mwanamuziki huyo anatangaza kustaafu yeye ndiye ameamua kuibuka upya katika fani hiyo.
Alisema kuwa nyimbo hiyo ameiimba akiwa amepata baraka zote kutoka kwa mzee huyo ambaye ndiye mtunzi wa nyimbo hiyo.
Aliongezea kuwa ataitambulisha nyimbo hiyo katika tamasha la kumuenzi Mzee huyo lililopangwa kufanyika Oktoba 1, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam