Akizungumza na mwandishi wa habari hii dhumuni la kumpa jina hilo mtoto huyo, H. Baba aliweka wazi kuwa ameamua kumpa jina hilo mtoto wake ikiwa ni jina la madini yanayopatikana nchini Tanzania tu.
Alisema kuwa madini hayo yanapatikana nchini na ndio yanayotangaza utaifa wa Tanzania hivyo kwa upande wake hajaamua kimakosa kumpa jina mtoto huyo.
"Unajua madini ya Tanzanite ndio pekee yanayoipatikana nchini huwezi ukayapata madini hayo nje ya nchi, ndio maana mtoto wangu nimempa jina hilo nikimfafanisha na madini hayo" alisema H. Baba.
Wasanii hao ambao wamefunga ndoa yao hivi karibuni huyo ndiye mtoto wao wa kwanza walioamua kumuita jina hilo ambapo wananamfafananisha na madini hayo yanayopatikana nchini.