Google PlusRSS FeedEmail

JAYDEE AENDELEA KUTESA MARIMBA MUSIC CHART



MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinumz amefanikiwa kuingiza nyimbo yake mpya ya 'My Number One' katika 'Marimba Music Chart' huku msanii wa kike Lady Jaydee akiwa ameendelee kushikilia nafasi ya kwanza.
Lady Jaydee ameendelea kuwafunika wasanii wenzake kwa wimbo wake wa Yahaya ambapo anazidi kushikilia nafasi ya kwanza kwa wiki 9 mfululizo huku msanii Ben Pol na wimbo wake Jikubali akiwa ameshikilia nafasi ya pili kwa wiki 9 mfululizo.
Nyimbo ya Yahaya ya msanii huyo Jaydee imevunja rekodi kwa mashabiki wake kuiomba kwenye radio mbalimbali hali inayosabisha kuendelea kubaki kuwa namba moja kwenye chati hiyo.

Nyimbo nyingine ambazo zimeonekana kufululiza kuwepo kwenye chati hiyo ni pamoja na nyimbo ya Mwana Fa pamoja na Ay 'Bila kukunja goti', Rama D 'Kama Huwezi'. hii ni kutokana na nyimbo hizo kufanya vizuri katika radio mbalimbali.

Marimba Music Chart (MMC) huandaliwa na mtandao wa Bongo 5, kila wiki kutokana na orodha za radio mbalimbali nchi ili kukuza muziki na kuibua changamoto kwa wasanii wa muziki wa bongo fleva.

MMC hutumia orodha za radio mbalimbali za Tanzania kuchuja na kupata orodha ya nyimbo zilizoingia katika orodha nyingi zaidi na kupata nyimbo 20, ambazo ndio zinazofikia kigezo cha kuingia katika Marimkba Music Chart.















This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging