Google PlusRSS FeedEmail

JAYDEE, AUNGANA NA WASANII WA AFRIKA

WASANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Nassibu Abdul 'Diamond Platnum' pamoja na Judith Wambura 'Jaydee' waungana na wasanii mbalimbali wa Afrika jijini Nairobi ndani ya Coke Studio.

Diamond na Jaydee wamekuwa ni miongoni mwa wasanii walioingia kurekodi kwenye studio hiyo ikiwa wameshirikiana na baadhi ya wasanii wenzao wa Afrika.

Jaydee alituma picha zilizomuonesha akiwa ndani ya studio hiyo jijini Nairobi akiwa na wasanii hao ambapo alituma picha ikimuonesha akiwa na Octopizzo wa Kenya.

Wasanii hao wamekuwa miongoni mwa wasanii waliingia ndani ya studio hiyo kurekodi nyimbo mmoja  itakayoimbwa na wasanii hao.

Coke Studio hujihusisha kurekodi live nyimbo za wasanii maarufu na kuzirudi kwa kuziboresha na kuzipiga kwa mitindo tofauti.

Studio hiyo ambayo imewaunganisha wasanii 24 kutoka nchi nane za Afrika.






This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging