Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo vya hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama anavyoonekana sasa.
Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi aishi na makovu kuliko kubeba matiti.
Akizungumza hali hiyo, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, alisema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenzi wake, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake.
Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo alisema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia.
Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanishwa, na hapo ndio mapenzi baina yao yalipowaka moto mpaka sasa.