MTANDAO WAMPONZA JUSTIN BIEBER
Msanii Justin Bieber amekana kutoa maneno yoyote ambayo yanauponda wimbo wowote ule. Kauli hiyo imetolewa na msanii huyo baada ya kudai kuwa kuna mtu alifungua ukurasa kwenye mtandao wa Youtube ambao unafanana kila kitu na ule wake.
Bieber alidai kuwa mtu huyo aliuweka wimbo unaoitwa 'What she Wants 2013' na kudai kuwa msanii huyo ameuponda, tukio hilo teyari limeshazungumzwa na vyombo kadhaa vya habari na ndio vilimfanya msanii huyo kuja juu na kuzungumzia tukio hilo.








