BAADA ya tuhuma za kubaka kumuandama msanii mwenye asili ya Jamaica anayeishi nchini Marekani Sean Kingston ajikuta akikosa dili za kumuingizia pesa, kwa kukosa show inayotarajiwa kufanyika mwanzoni wa mwanzo huu. Msanii huyo amejikuta katika wakati mgumu baada ya taarifa juu ya msichana aliyemtuhumu kumbaka kusambaa wiki iliyopita.
Mtandao wa TMZ ulilipoti kuwa msanii huyo alitarajiwa kutumbuiza Septembar 7 mwaka huu katika chuo cha Western Ontario kilichokuwepo nchini Canada, lakini kutokana na tuhuma hiyo chuo hicho kilibadilisha
maamuzi hayo.
Chuo hicho kilidai kuwa kimeamua kusitisha msanii huyo kuwatumbuiza wanafunzi wapya kwa madai kuwa
chuo hicho hakiungi mkono masuala ya aina hiyo.
Sean Kingston anatuhumiwa kumbaka kwa kumchangia msichana mmoja akiwa na walinzi wake wawili ambapo kitendo hiko kilifanyika mnamo mwaka 2010.








