
Mtayarishaji wa filamu hiyo Hashim Kambi ‘Ramsey’ amesema kuwa msanii huyo Van Vicker ambaye alimwalika kuja kushiriki katika filamu yake hiyo ameigiza katika filamu vizuri sana na kuwapa somo wao, lakini hadi anaondoka filamu hiyo ilikosa jina kwa sababu mtunzi wa filamu hiyo Leah Mwendamseke ‘Lamata’ alitaja jina ambalo kuna sinema .
“Unajua nilisoma hadithi yake na kuipenda kwa hiyo alivyokuja Van Vicker tualianza kurekodi Director Simon Mwakifwamba wangu akaliona lile jina na ambalo ni Mtandao na kubaini kuna filamu hiyo, baadaye Lamata akasema iitwe Network kumbe tayari kuna sinema ya MFDI ipo kwa jina hilo,”anasema Ramsey’.
Hadi inamalizika kurekodiwa sinema haikuwa na jina hivyo wanamsubiri Van Vicker awatungie jina kwani wakati akiondoka aliwashauri wasubiri akifika Ghana atangalia jina la kuipa na wao kutumia, changamoto ni kubwa sana hadi jina la filamu linatoka nje wakati watunzi wapo hapa kuna changamoto katika tasnia ya filamu