Jina Kamili : Kala Masoud
Jina la Kisanii : Kala Pina
Msanii wa miondoko : Kala Pina ni msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini ambapo yupo katika kundi la Kikosi cha mizinga.
Mbali na muziki : Msanii wa Hip Hop nchini Kala Pina pia anajishughurisha na masuala ya Siasa na kilimo ambapo alizama kwenye siasa huku akiamini kuwa Tanzania ni nchi ya demokrasia.
Mchakato wa siasa alianza lini ? Alijiingiza katika masuala ya siasa mnamo mwaka 1995 ambapo alijiiunga na chama cha Wananchi Cuf huku akiwa mwanachama hai kwa kuugawa muda wake kuhudhuria vikao mbalimbali vya kichama.
Hali ya uongozi ndani ya chama: Mnamo mwaka 2011 aliweza kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambapo aliweza kupata nafasi ya kuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana CUF.
Mchango ndani ya chama : Anaamini ndani ya chama hicho anamchango mkubwa ikiwemo wa kuhamasisha vijana wengi kujiunga ndani ya chama hicho ili kuleta changamoto kwa vijana hususani suala la kimaendeleo.
Mkulima : Mbali na kujiunga na masuala ya chama pia anajishughurisha na shughuri za kilimo cha umwagiliaji huku akiamini kuwa kuongeza kipato kwenye upande huo.
Maeneo : Anajishughurisha na kilimo hicho maeneo ya Rufiji mkoa wa Pwani, ambapo analima kilimo cha umwagiliaji mazao ya nafaka kwa ajili ya biashara.
Elimu yake : Amejikita katika suala hilo kutokana na elimu aliyoipata alipokuwa shule kwani alisoma masomo ya kilimo.