MSANII wa muziki wa Hip Hop nchini Kala Jeremiah amepata shavu baada ya kuingia mkataba na kampuni inayotengeneza vinywaji baridi ya Pepsi (SBC) kama balozi wao.
Msanii huyo ameingia mkataba na kampuni hiyo ya SBC kwa miezi sita ya kufanya kazi na kampuni hiyo kama balozi wao.
Akizungumza na jarida hii Kala aliweka wazi kuwa kwake ni hatua kubwa kupata mkataba huo hali inayopelekea kuonesha kuwa muziki wake umekubalika kwa jamii.
Aliweka wazi kuwa wasanii wa Hip hop ni kati ya wasanii wanaoimba ujumbe unaougusa jamii moja kwa moja hivyo hali hiyo inawapa nafasi ya kuwa karibu zaidi na jamii.
"Kuingia mkataba na kampuni hiyo kwangu ni hatua kubwa kwa kuona sasa muziki wangu umeanza kukubalika kwa jamii yangu na watu kuelewa kazi yangu" alisema Kala.
Msanii huyo aliendelea kuweka wazi kuwa juhudi, bidii na nidhamu ya kazi ndiyo siri kubwa anayoitumia inayomsababisha yeye kuendelea kufanya vizuri katika soko la muziki nchini.








