Google PlusRSS FeedEmail

MAMA KANUMBA ATISHIA KUMFUNGA NABII KAIRUKI

                                              Frola Mtegoa 601

Flora  Mtegoa mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji nyota filamu wa Bongo marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na tabia ya mtu anayejiita Nabii George Kairuki kwa kutumia jina na kifo cha marehemu mwanaye kama njia ya kujitengenezea fedha na umaarufu, mama Kanumba anasema kuwa awali Kairuki alitumia msiba wa mwanaye katika kuongelea vitu ambavyo hata familia haivijui isipo kuwa yeye pekee yake.




“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba.

Frola Mtegoa

Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.
.
Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging